Monday, August 29, 2016

Simbachawene: Serikali haina nia mbaya na wananchi

SimbachaweneWaziri wa nchi ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa, George Simbachawene amesema kuwa dhamira ya Rais Dkt John Magufuli ni kuwatumikia wananchi na kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwa Watanzania wote.

Amezungumza hayo katika kipindi cha “TUNATEKELEZA” kinachoandaliwa na HABARI MAELEZO kinachorushwa na TBC 1. Alisema kuwa serikali ipo kwaajili ya kuwatumikia wananchi katika kila sekta na kutatua changamoto wanazokumbana nazo wananchi.
“Kupitia falsafa yetu ya hapa kazi tu tutahakikisha tunawaletea wananchi maendeleo katika ilani ya 2015 -2020 ya chama cha mapinduzi kilicho na serikali”, alisema Simbachawene.
Dk Simbachawene aliwahakikishia wananchi kuwa lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuwatimizia wananchi ahadi ilizowaahidi kwakuwa wanayo dhamira ya kweli ya kuwatimizia wananchi.
Aliongezea kwa kusema kuwa Rais Magufuli ameamua kuleta mabadiliko ya kweli katika nchi, ambayo yanalenga kuwabana wabadhirifu na mali za umma na kurejesha nidhamu kazini jambo ambalo limeanza kuonekana katika ofisi mbalimbali za umma.

BY: EMMY MWAIPOPO

Nimeshafanya makubwa hapa nyumbani, nahitaji kwenda kimataifa- Dully Sykes

dully-12Msanii mkongwe wa muziki wa bongofleva, Dully Sykes baada ya kufanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Inde’ amesema kilichobaki kwenye muziki wake ni kufungua milango ya kwenda kimataifa.
Akiongea na Bongo5 Jumanne hii, Dullly amesema kufanya vizuri nyumbani kutamsaidia kutoboa zaidi kimataifa kwa kuwa mashabiki wa nyumbani ndio wenye nguvu ya kumpush kwenda kimataifa zaidi.
“Kwa sasa plan yangu ni kwenda kifataifa, tayari nimeshafanya kila kitu kwenye huu muziki,” alisema Dully Sykes “Ninamashabiki ambao kwa sasa ni wazee na wengine wameshakufa na bado naendelea kutengeneza wapya, kwa hiyo kwangu mimi vingi nimeshafanya hapa nyumbani, sasa nataka kwenda mbele zaidi,”